Shule ya Sekondari Santa Kagwa.

Kauli mbiu yetu ni "LENGA JUU"

Fanya kila uwezalo kwa uwezo wako wote na jitahidi kufanya vizuri zaidi, kuthubutu ni tunu ya mafanikio.


WHO WE ARE - Sisi ni nani

Shule hii ya Sekondari Santa Kagwa inamilikiwa na mwalimu Linus Mizengo, ilianza rasmi mnamo tarehe 09/01/2010; imesajiliwa mwaka 2013 kwa namba S.4667 na namba ya kituo cha mtihani S.5053 na P.5053. Shule ipo Sumbawanga mjini eneo la Kisiwani km. 4 kutoka stendi kuu ya mabasi Sumbawanga mjini. Shule inapokea wanafunzi wa jinsia zote kwa Tanzania na nje ya Tanzania

SERA YA ELIMU - SANTA KAGWA SEKONDARI

DIRA (Vision)

Kuwa na watu au wanajamii walioelimika kwa kiwango cha juu mwenye maadili stahiki, stadi na mwelekeo mwema kimwenendo kwa kadiri ya mila na desturi za jamii yetu. Zaidi awe mahiri na jasiri aliye tayari kushiriki kwa ufanisi katika kuyafikia malengo ya maendeleo yaliyowekwa na taasisi yetu na taifa kwa ujumla.

DHIMA (Mission)

Kuwezesha/kutoa elimu bora na maadili mema kwa watu kwa kushirikiana na wadau wengine.

TUNU (Values)

Kuthamini na kuzingatia mila na desturi za kitanzania na Afrika kwa ujumla hususani mkoa wa Rukwa.

MALENGO YA ELIMU (Aims/goals)

Shabaha ya elimu ni kuleta mabadiliko chanya yatakayo-msaidia binadamu aweze kuishi vizuri na kujiletea maendeleo ya kweli yenye kutunza utu na thamani yake.

UONGOZI WA SHULE


master avatar

Mwl. Linus Mizengo

Mkurugenzi wa shule Santa Kagwa sekondari

master avatar

Mr. Tenson Mzumbwe

Mkuu wa shule Santa Kagwa Sekondari
+255 763 064 290

master avatar

Mr. Zacharia Mwasenga

Makamu mkuu wa shule na msimamizi wa malezi ya watoto wa kike Santa Kagwa sekondari
+255 757 767 665

master avatar

Mr John John

Makamu mkuu wa shule na msimamizi wa malezi ya watoto wa kiume Santa Kagwa sekondari
+255 758 222 906